Leo alfajiri game ya muziki wa kizazi kipya imempoteza nyota
wake ambaye alikua member wa kundi la TMK Wanaume halisi.The late Baraka
Sekela, kwa jina la stage ni BK, ambaye yeye ni moja kati ya waasisi wa kundi
la TMK Family, hata makao makuu ya kundi hilo yalikua nyumbani kwa wazazi wake
karibu na uwanja wa taifa wilaya ya Temeke, jijini dar es salaam.
Marehemu bk
alikua anaumwa, hadi mauti yanamkuta alikua amelazwa hospitali ya rufaa ya
muhimbili.
"Kwa
mujibu wa rafiki yake wa karibu sana Hassan Omandi, marehem alikua
anaumwa tumbo kwa takribani siku tisa na kuambiwa ana taifod katika
hospitali aliyoenda kufanya vipimo, lakini baada ya kuanza dozi
akazidiwa kabisa, ikabidi twende hospitali ya Temeke, kule wakaona ni
tatizo kubwa na kumpeleka Muhimbili, ndio huko akaambiwa ini lake
linamatatizo ya kuvimba."amesema rafiki yake wa karibu anaeitwa Hassan
Omande
No comments:
Post a Comment