Miss
kutoka Philippines Megan Young ndio amevishwa taji la Miss World 2013
iliyofanyika usiku wa jumamosi, Bali Nusa Dua Convention Center
Indonesia.
"I promise to be the best Miss World ever," Alisema Miss Megan baada ya kuvishwa taji hilo na miss world 2012, Wenxia Yu.
Young,
ambae alizaliwa nchini Marekani amewashinda wasichana wengine 126
walioshiriki katika shindano hili ambalo ni la 63 tangu kuanzishwa.
Megan
alihamia Philippines alipokuwa na miaka 10 na amekuwa akiishi huko
mpaka hivi sasa, na kufanya kazi kama muigizaji na mtangazaji wa
Televishen.
Miss France, Marine Lorphelin, 20, amekamata nafasi ya pili na Miss Ghana Carranzar Naa Okailey amekuwa wa tatu.
Miss
Tanzania alieshiriki shindano hilo mwaka huu, Brigitte Alfred, ameibuka
nafasi ya tatu katika shindano la Beauty with a purpose ikiwa ni
shindano linaloenda sambamba na shindano la Miss World
No comments:
Post a Comment