Tanzanite ambae pia jina lake linaendana na jina la Dimond (yote madini) alifunguka haya katika interview aliyofanya na Lucas Maziku, mtangazaji wa radio SAUT ya jijini mwanza.
“ Dah, unajua msema kweli ni mpenzi wa Mungu na siwezi kuficha kwa sababu nikificha ntakuwa sijengi nabomoa, halafu mimi naweza kusema ni ulimbukeni tu wa baadhi ya wasanii wa Tanzania. Mimi nilipata matatizo flani hivi nilikuwa naugua tangu kipindi kile nimeachia wimbo wa wachawi na wanga.
Yeah, nimeugua kwa kipindi kirefu ugonjwa ambao yaani tumehangaika sana hospitali bila kupata matatizo yoyote kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na kifua, wazazi wangu walikuwa wanajua labda ilikuwa TB kwa sababu nilikuwa na hali mbaya kiukweli.
Nilikuwa nimepungua nilikuwa nakohoa, nilikuwa natoa makohozi yenye damu. Lakini hayo makohozi yalikuwa yanashangaza sana kwa sababu yalikuwa yanatoa nywele, nywele za binadamu za kichwani.” Alisema Tanzanite.
Aliendelea kufunguka “ Hali ilikuwa mbaya ikabidi wazazi wangu waangalie upande wa pili (waganga wa kienyeji), sasa tulivyoangalia upande wa pili napo mambo yakawa magumu, lakini kila sehemu tuliyokuwa tunaenda, si unajua tena mambo ya upande wa pili siyaamini moja kwa moja lakini kwa nini kwamba kila sehemu niliyokuwa naenda nilikuwa naambiwa mtu flani, mtu flani, mtu flani...
Tumeenda sehemu kama 9 tena mikoa tofauti, umeelewa, lakini kila sehemu tunayoenda tulikuwa tunaambiwa bwana Nasibu Abdul ndiye anaefanya mambo haya, sasa Nasibu Abdul ni Diamond.
Na nikiangalia kisa labda au sababu, hao wazee walikuwa wananambia kuna vitu mlikuwa mnagombania na huyo mtu, hao wazee wenyewe hawajui kwamba ni vitu gani nilikuwa nagombania na huyo mtu, umenielewa vizuri eeh.” That’s Tanzanite akifunguka.
Jamaa kafunguka mengi, ikiwa ni pamoja na kilichomkuta alipokutana uso kwa uso na bwana Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platinum, ilikuwa ni full vitisho kwa mujibu wa Tanzanite mwenyewe.
No comments:
Post a Comment