Baada ya wanasheria wa msanii huyo ambao ni Peter kibatala, Kennedy
Fungamtama na
Fulgence Massawe, kutuma maombi ya dhamana ya kesi ya Lulu ili isomwe
haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu mahabusu, sasa habari
zilizotoka hivi punde kutoka mahakama kuu zinasema lulu ametakiwa
kukamilisha masharti aliyopewa, ikiwa ni kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezi, na
wafadhili wawili kuweka bondi ya Shilingi mil 20 kila mmoja...masharti hayo yakikamilika leo hii ataachiwa huru kuwa uraiani.
Upande wa familia ya Lulu
umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo
wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo
masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake
itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba
uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho
kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani
Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya
masharti.
No comments:
Post a Comment