Tuzo za Ballon d'Or zenyewe zimekuwa zikikosolewa sana siku za hivi karibuni. Wakati hakuna anayeweza kupinga ushindi wa Messi na washindi wa siku za nyuma, kuna suala la namna zoezi zima la kupata mshindi ndio lenye utata. Utaratibu wa upigaji kura upo kisiasa zaidi na matakwa binafsi ya wapiga kura.
Ushindani unakuwa haupo sawa kwa sababu makocha na manahodha wanawapigia kura marafiki zao wanaocheza timu za taifa na vilabu. Pia mahusiano baina ya nchi za America Kusini, Scandinavia, nchi za Uingereza siku zote zitaleta tatizo kwenye kupiga kura. Ikiwa Jack Wilshare au Joe Hart atakuwa akigombea tuzo hiyo, we unadhani England, Wales, Ireland na Scotland zitampigia kura nani?
Wengine wanaweza kusema kura zimetokana na viwango vya wachezaji kwenye michuano mikubwa kama vile Euro 2012. Lakini hili linawapa faida kubwa wachezaji wa bara la ulaya ambao wanapata nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo. Tatizo kama hilo pia kwenye michuano ya Copa America. Kitu kingine, wakati Blatter na Platini wamekuwa wakizijadili nchi kama England, klabu za kiingereza, na premier league kwa kutoa maoni hasi, siku zote kutakuwepo hali ya kutokueleweka inayozunguka upendeleo kwenye ligi fulani, nchi na wachezaji.
Mwisho, ni vigumu kuitetea tuzo hii ambayo wachezaji kama Thierry Henry, Maldini, Baresi, Nesta na Raul hawakuwahi kushinda. Pia inaonekana imekuwa tuzo ya wachezaji wanaocheza nafasi za ushambuliaji kila mwaka.
Timu bora ya mwaka uliopita, kama ilivyochaguliwa na kura za wanasoka wapatao 45,000 kutoka ulimwenguni kote, yote imetokana na wachezaji wanaocheza kwenye ligi kuu ya Spain La Liga, kulikuwepo na mchezaji mmoja tu wa Atletico Madrid Radamel Falcao, wengine wote wakitoka kwenye vilabu vya Real Madrid na Barcelona. Ligi kuu ya England ambayo mara nyingi imekuwa ikitajwa kuwa ndio 'ligi bora duniani' kwa wachezaji, makocha na mashabiki kutokana na ushindani mkubwa kwenye ligi na mafanikio ya vilabu kwenye champions league kwa miaka mingi sasa. Pia kutokana na mafanikio ya Bundesiliga msimu huu na uliopita kwenye UCL, wengi wanasema kwamba ligi hiyo nayo ni bora duniani. Vyovyote vile, ni jambo lisilofikirika , au la kijinga, ama la kipuuzi ama vyovyote unavyoweza kuliita kuona hakuna mchezaji yoyte kutoka kwenye Bundesiliga na EPL aliyechaguliwa kuingia kwenye FIFPro World XI.
Kila mtu ana mawazo yake na wachezaji wake anaowapenda lakini hisia za mashabiki wa soka kutoka ulimwenguni kote. Kukosekana kwa mchezaji japo mmoja wa Manchester City kumeleta mjadala sana, hasa kwa mchezaji Vincent Kompany, na Yaya Toure. Hakuna anayeweza kutetea ni vipi nahodha wa mabingwa wa England, yupo nyuma ya Gerard Pique, ambaye mafanikio makubwa binafsi yalitoka nje ya uwanja akiwa na Shakira. Alikuwa na muda mzuri wa kufarahia maisha na mtoto mzuri wa kikolombia na akakosa msimu karibia nusu msimu wa La Liga 2011-12 na alikuwa hayupo kwenye fomu nzuri wakati patna wake Carles Puyol alipopata majeruhi.
Pia ingekuwa ngumu kutetea hoja ya kikosi bora cha FIFA ambacho hakijatoa hata mchezaji mmoja aliyeshiriki kwenye fainali ya UEFA Champions League 2012. Ndio, Chelsea walikuwa na bahati nzuri kwenye mechi nyingi mpaka walipoenda kuchukua ubingwa, lakini kama Blatter na Platini wataendelea kutoitendea haki Premier League kutokana na matumizi makubwa ya fedha kama wasemavyo wakuu wao hao wa taasisi kubwa za soka duniani, na huku wakisisitza kwamba Champions League inaonyesha ubora wa kweli wa timu, basi Drogba, Cech, na Ashley Cole hawastahili kutambuliwa kwa ubora wao??? Ashley Cole anatajwa na wengi kwamba ndio beki bora wa kushoto, na huku ubingwa wa ligi ya mabingwa wa ulaya ukiwa himaya yake, kwa hakika alitakiwa kupewa nafasi mbelel ya beki wa Real Madrid Marcelo.
Kwa wengine, uchaguzi uliowashangaza zaidi ni Dani Alves kwenye beki wa upande wa kulia. Wakati wa mwanzo wa ligi msimu uliopita, mbrazili alikuwa kweli beki bora wa kulia duniani. Lakini 2012 ulikuwa mwaka m'baya zaidi kwake tangu awasili nchini Hispania, alipatwa na matatizo chini ya Guardiola na baadae akawa anawekwa benchi na Tito Vilanova. Kuwepo kwake ndani ya kikosi cha wachezaji bora wa 2012 ni ushahidi tosha wa jinsi hii timu ilivyoundwa kwa kujuana, majina yanayojulikana yaliyochaguliwa na watu ambao hawaangalii soka vizuri au walifanya kusudi tu.
Tusi la mwisho katika kikosi hiki, lilikuwa ni kukosekana kwa jina la Andrea Pirlo. Mchawi huyu wa soka wa kiitaliano atakumbukwa kwenye historia kama mmoja wa viungo bora wa kati wa muda wote, mwaka 2012 ulikuwa ndio mwaka wake bora akiiongoza Juventus kunyakua Scudetto bila kufungwa mechi hata moja, kabla ya kushinda tuzo tatu za mchezaji bora wa mechi wakati akiiongoza Italy kwenda fainali ya EURO 2012. katika msimu huu unaoendelea sasa kiwango chake bado ni maradufu.
Mwisho kabisa tuzo za Ballon d'Or zimeshapoteza maana kutokana na siasa kuingizwa kati kati.
No comments:
Post a Comment