flash3

Wednesday, 17 April 2013

DAIMA UTAKUMBUKWA LEGENDARY FATUMA BARAKA (BI. KIDUDE)

bikidude
Taarifa za kuaminika saa chache zilizopita kutoka Visiwani Zanzibar zimehakiki kuwa gwiji la muziki barani Afrika Fatuma Binti Baraka maarufu Bi Kidude, amefariki dunia.
Habari kutoka nyumbani kwa familia ya marehemu zinasema kuwa Legendary Bi.Kidude atazikwa siku ya kesho huko visiwani Zanzibar.
Bi Kidude ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika, ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu.
Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi.
Marehemu Bi Kidude amewahi kusema kuwa hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya.
Gonga continue reading kuendelea..

Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad.

MFAHAMU ROLE MODEL WA MAREHEMU FATMA BINTI BARAKA (BI. KIDUDE)

siti_binti_saad


Historia ya Marehemu Bi Kidude inaonyesha kuwa mkongwe huyo alianza mziki tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad.
Marehemu Bi kidude enzi za uhai wake amewahi kufunguka kuwa wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti.
Gonga continue reading kuendelea..

Siti binti Saad alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari mwaka 1880. Alipozaliwa alipewa jina la ‘Mtumwa’ hii ni kwa vile alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na mkabaila mmoja wa kiarabu.
Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari. Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.
Kama waswahili wasemavyo ‘kuzaliwa masikini si kufa masikini’ Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji.
Kipaji hiki kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza.
Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo. Alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.
Fahamu zaidi kuhusu Siti binti Assad kupitia kamusi ya elezo huru, ambayo ina makala maalumu kuhusu legendary huyo.

No comments:

Post a Comment