Watunga sheria wa Ufaransa wamehalalisha ndoa za jinsia moja baada ya
miezi ya mjadala mkali na maandamano ya mitaani yaliyopelekea mamia kwa
maelfu kuja Paris.
kura 331 - 225 za siku ya juma nne zimeangukia kwa walio wengi ndani ya
bunge ambao ni Socialist. waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane
Taubira,amesema ndoa ya kwanza kufungwa itaweza kuwa mapema mwezi june.
wanaopinga sheria hiyo wanasema, Ufaransa haiko tayari kuhalalisha ndoa
za jinsia moja, na kura zinaonyesha kuwa wafaransa wamejitenga juuu ya
swala hilo.
mamia ya askari walimwagwa nje ya viwanja vya bunge kabla ya kura hizo
kupigwa, kwa maandalizi ya kama kungekuwa na maandamano kuzunguka jengo
la bunge na kando kando ya mto Seine.
Ufaransa
ni nchi ya 14 ya kuhalalisha ndoa za mashoga, na kura ya Jumanne
imekuja wiki moja baada ya New Zealand - kwa utata kidogo sana -
kuruhusiwa wanandoa wa jinsi moja kuoana.
No comments:
Post a Comment