Baada ya kifo cha ghafla cha
Rais John Atta Mills wa Ghana jana, saa chache baadae Makamu wa rais
John Mahama ndio amekabidhiwa madaraka kwa sasa.
Kuhusu chanzo cha kifo cha
Mills, BBC wamesema taarifa kutoka ofisi ya rais zinasema alifariki
ghafla baada ya kupelekwa hospitali Jumatatu usiku na inaaminika aliugua
ugonjwa wa kansa.
Kifo cha rais wa taifa hilo la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kugombea tena urais.
Rais Attah Mills ambaye
husafiri mara kwa mara kwenda ng’ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi
baada ya kupelekwa hospitali Accra , Ghana ambapo ni siku chache tu
zimepita toka apelekwe Marekani kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Ghana ilikuwa inatarajiwa
kwenda katika uchaguzi mkuu Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills
alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea hiyo nafasi, wakati wa uongozi
wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
John Atta Mills ambae
alianzisha uchimbaji wa mafuta nchini Ghana amefariki dunia akiwa na
umri wa miaka 68 na amefariki dunia siku tatu tu baada ya kusherehekea
siku yake ya kuzaliwa July 21.
No comments:
Post a Comment