Siku zikiwa zinahesabika ili
msanii Mfalme wa Rymes Afande selle kutangaza chama atakachogombea nacho
Ubunge 2015 Morogoro Mjini, mkongwe huyu amekubali kuwataja wanasiasa
ambao ndio wanamvutia, wanampa hamu na ushawishi wa hiyo kazi kutokana
na wanayoyafanya.
Afande anaesema anayajua
machungu ya wanamoro amekiri kwamba wanaomvutia kwenye siasa ni wengi
lakini wachache wao sana sana ni Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Halima Mdee wa Kawe na Burhani wa Lindi.
Amesema “mtu kama Zitto Kabwe
ni mtu ambae ananipigia simu mara nyingi nikiwa na masahibu yangu
ananishauri, namuheshimu sana na nafasi hii naitumia kumshukuru, yuko
dada Halima Mdee wananionyesha kitu flani ambacho ninaweza kukifanya
vilevile, kuna wabunge vijana kama Baruani kutoka Lindi japo ni Albino
lakini ameonyesha kwamba Albino anaweza kuwa kiongozi mzuri kuliko hata
watu wasio na ulemavu, wako wengi wananivutia hasa kutoka vyama vya
upinzani”
Kwenye interview yake ya May
2012 na AMPLIFAYA, Afande alisema kuna vyama saba vya kisiasa
vilivyomuita ajiunge navyo kugombea Ubunge lakini viwili ndio vyenye
nafasi kubwa, kimoja kati ya CHADEMA au C.U.F
Alisema “kimsingi ndio vyama
ambavyo hata namna ya kuvionganisha ningetamani siku moja viwe na sera
moja na kuungana kuipigania nchi hii kwa sababu siamini kama kimoja bila
kingine kati ya hivyo viwili kinaweza kuliangusha hili dudu kubwa
ambalo lipo madarakani”
No comments:
Post a Comment