Huyu ni Mwanamuziki anayetokelezea maeneo ya Kilifi maarufu kama Kilifonia, miaka ya 2003-2005 amewahi kuwa tishio katika fani ya muziki jambo ambalo kwa sasa linashangaza wengi kuwa haonekani tena katika ulinogo huu wa Mombasani.
Pat C alijuliana na nyimbo kama vile Nakuhenza Muche, Usiulize, Dede na Nyingine nyingi, amewahi kupiga Kolabo na wana muziki ambao mpaka leo wana tamba kama vile, Susumila, Lai, Mchafuzi, Trick B na nyimbo zenyewe zikawa 'Talk Of Town'.
Swali limebaki, 'AMEPOTELEA WAPI'
Kulingana na utafiti wa mtandao huu, umewahi kugundua kuwa wanamuziki wengi hapa pwani huingia mitini pindi tu baada ya kupata majiko.......JEE KWA PAT C, HIYO NDIO SABABU.
Kwa mengi zaidi endelea kutazama mtandao huu, umjue Pat C alipo.
No comments:
Post a Comment