Rais Mwai Kibaki anatarajiwa kufika mjini
Mombasa Alhamisi kufungua rasmi maonyesho ya kilimo ya Mombasa, wakati
ambapo mji huu unashuhudia vurugu zinazosababishwa na vijana wanaopinga
kuuawa kwa mhubiri wa dini ya kiislamu Aboud Rogo Mohammed.
Mapema
Leo, ghasia zimezuka upya katika mitaa ya Majengo, Saba Saba na
Makupa ambapo watu watatu wamejeruhiwa vibaya.
Mkuu wa polisi mkoani
Pwani Aggrey Adoli amekanusha vikali madai kuwa mke wa mhubiri huyo
ameaga dunia akisema amelazwa.
Haniya Saaid Sagaar anauguza jeraha la
risasi kwenye mguu wake. Aidha, Adoli amewakosoa wafwasi wa muhubiri
huyo kwa kuwanyang'anya maafisa wa polisi mwili wa marehemu na hivyo
kuhujumu uchungunzi wa kifo hicho.
Polisi wamekuwa wakikabiliana na
vijana wanaozua vurugu katika barabara za Nkrumah, Nyerere, Digo, Posta
na Moi jijini humu. Hali hiyo imesababisha maduka kadhaa kufungwa baada
ya wamiliki kuhofia usalama wao huku wengine wakiwa wameporwa pesa na
mali nyinginezo. `
No comments:
Post a Comment