mwanamke mwenye umri mdogo Adeola Joseph, aliemzika mtoto wake pekee
katika nyumba yake iliyoko Osogbo kwa siku mbili mwaka 2012,
amehukumiwa kifungo cha miaka6 jela. Jaji Olusola Aluko, alitoa amri kwa
mwanamke huyo mwenye miaka 18 kifungo hicho kikiambatana na kazi
ngumu, na kudai kuwa mtuhumiwa huyo ambae haonekani kutubu kwa
alichokifanya, hastahili kuishi na binaadamu wengine.
mwanamke huyo ambae amethibitishwa na madaktari kuwa na akili zilizo
timamu wakati wa mashtaka yake, ameishi na mtoto huyo kwa miaka 2, na
ameshafanya majaribio kadhaa ya kumuua mtoto huyo anaeitwa Fatia,
jaribio la kwanza lilikua November 2011 pale alipomuwekea sumu kwenye
chakula, na inasemekana pia jaribio la pili lilikua december 2012 mwaka
jana wakati mama huyo alipomtupa mtoto pembezoni mwa mto Osun lakini
wapita njia walimuokoa mtoto huyo na kumpeleka kwenye kituo cha watoto
wasio na mama ambapo baadae alirudishwa kwa mama yake.
mama huyo na mtoto waliishi pamoja mpaka pale alipofanya jaribio la tatu
kumuua kwa kumzika akiwa hai, ambapo wasamaria wema walimuokoa baada ya
kukaa ndani ya kaburi hilo kwa siku mbili. wananchi walimiminika
kumuangalia mtoto huyo ambae amekwepa kifo kwa majaribio matatu
yaliyofanywa na mama yake.
Josph aliiambia mahakama sababu zilizomfanya kufanya ukatilio huo ni
ndugu zake kutokupendezwa na ndoa yake na baba wa mtoto huyo na kuamua
kuishi mwenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yoyote. Pia mshtakiwa huyo
kaiambia mahakama kuwa aliamua kumuua mtoto huyo kutokana na uamuzi
wake wa kuhamia Lagos kwa ajili ya kutafuta kazi, na asinge weza
kukabiliana na majukumu ya kazi na kulea mtoto.
kwa sasa mama huyu amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kazi ngumu.
No comments:
Post a Comment