flash3

Monday 9 July 2012

Umri Mdogo Sio Kigezo katika Majumba Ya Habari...........

Ukidhani kuwa Umri mdogo katika fani ya utangazaji nikipingamizi, basi umenoa.
Pwani Fm ilijipata ikipanda na kuendelea kufanya vyema katika soko la mashabiki na mauzo ya kimatangazo baada ya kubahatika na talanta ya Eric Munene John maarufu kama Dj Gates.
Sio zaidi ya miaka mitatu tangu aungane na pwani Fm, lakini katika vipindi alivyohusishwa na Redio hiyo maarufu mkoani pwani, amejipata akiolea katika dau la sifa na kuzidi kupandisha hadhi ya Kituo hicho cha redio.
 Mawazo yake mengi aliyofanikiwa kuyaleta katika ulingo huu wa fani ya Redio lakushangaza zaidi ni kuwa yameendelea kuigwa na baadhi ya majumba ya habari mkoani pwani nchi na East Afrika Nzima kwa ujumla.
Katika taaluma hii ya utangazaji Gates amejipata kuwa mdau muhumu sana katika ujenzi wa muziki wa jimbo la pwani, mziki ambao kila uchao unakuwa kwa kasi kubwa.
Mtangazi huyu hutumia msemo( mziki na wanamuziki wa pwani wanahitaji malezi ya kila mmoja waye yule ili kuwafanya wajifae katika maisha yao ya kila uchao...........)
 Akihojiwa na mtandao huu, mwiba huyu wa Redio uliokuwa tishio kwa wengi waliobobea katika fani hii, amesema kuwa hataachwa nyuma kuwa mbunifu zaidi huku akisema kuwa utangazaji kwake ni kipaji na haoni kuacha kufanya kazi hiyo.
Kwa sasa anaendelea na kipindi Mashav Mashav University kianzacho masaa ya saa tatu asubuhi hadi sa sita mchana.
Mbali na utangazaji na mwalimu wa masanturi yaani Dj, Gates ni mwandalizi wa matafrija mkoani pwani, Kenya na East Afrika Kwa ujumla..........

No comments:

Post a Comment