Inawezekana kuwa ni njia mpya ya
kutaka kuteka watu nyara na kutengeneza hela kwa aina mpya ya biashara baada
ya kukaa kwenye muziki kwa miaka ishirini, huu ni uamuzi wa rapper Snoop
Dogg ambaye sasa amebadilisha jina na kujiita Snoop Lion.
Ametangaza kuanza kuimba muziki
wa Reggae anaouita muziki wa upendo, muziki atakao kuwa huru kuuperform
hata kwa bibi, babu na watoto kwa sababu una mapokezi kwa marika yote
tofauti na muziki wake wa kigumu alioufanya kabla.
Snoop Lion amesema alichofahamu
kutoka kwa Marasta ni kwamba sio dini kama watu wanavyofikiria pia
kuhusu jinsi wanavyoishi, amegundua kitu kingine tofauti pamoja na
kusisitiza kwamba amekuwa na rasta kwa kipindi kirefu lakini alikuwa
hajafungua jicho la tatu ili kuligundua hilo, ila baada ya kufungua ndio
amefahamu.
(picha zake za awali kabla ya maamuzi yake ya kufanya muziki wa rege.)
Kubadili jina na kuanza
kufanya muziki wa Reggae hakuwa amekupanga, anasema ni hisia zilikuja tu
na akaamua kuzifata, baada ya hapo ndio akasafiri mkapa Jamaica na
kuingia kwenye studio ambayo aliiagiza imtengenezee kazi za ukweli za
Reggae ambazo alizifurahia na kuzifanyia kazi.
Snoop mwenye umri wa miaka 40
ambae kipimo cha DNA kilionyesha kwamba asili yake sio Asia bali ni
Africa 75%, 23% Native American na 6% European amesema haimaanishi
kwamba muziki wa rap aliokuwa akiufanya mwanzo ni mbaya na kwamba
anauacha bali anafanya muziki ulio kwenye hisia zake kwa sasa ambao ni
reggae.
No comments:
Post a Comment