flash3

Saturday 7 July 2012

Susumila apongeza vituo vya redio vya mkoa wa pwani...........

Mwimbaji Yusuf Kombo maarufu kama Susumila hii leo amejitokeza wazi wazi na kusema kuwa vituo vya redio mkoani pwani vina faa kupongezwa kwa kazi wanayoifanya katika ujenzi wa fani ya muziki wa pwani.
Akinukuliwa kupitia mtandao wa Facebook, alipokuwa akijibu kauli ya Jamal Abdallah mmomja katika Facebook, susu adaisha kuwa vituo vya pwani vitabaki kuwa jicho na njia ya ufanisi wa mwanamuziki yeyote yule kutoka pwani.
Wakati uo huo mwana wa Kombo hakuachwa nyuma kuwakashifu wale wanaoponda vituo hivyo huku akisisitiza kuwa wapinzani hawana nia ya kujenga ispokuwa kuvunja.
Aidha amewaomba wale wote walio na moyo wa kuujenga mziki wa pwani wasirudi nyuma.
Kwa sasa Susu anaendelea kufanya vyema katika soko la muziki ikizingatiwa kuwa wimbo wake mpya YULEE!!!!!!!!!!!!!!!!! alioutengeneza katika studio za Crack Sound Kilifi uko katika nafasi ya kwanza katika chart ya Tafrija Remix Kipindi kimoja maarufu katika redio Pwani Fm Msa.

No comments:

Post a Comment