MAMIA
ya wakazi wa Kijiji cha Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu, juzi
walifurika katika Kitongoji cha Mabulugu kumshuhudia mwanamke Ngulima
Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa
katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani humo.
Inadaiwa kuwa
mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache
baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake. Habari zaidi
kutoka katika kitongoji hicho zinasema mwanamke huyo bado amefungiwa
ndani ya nyumba yake akifanyiwa dawa za kienyeji ili arudie katika hali
yake ya kawaida, kwani kwa sasa anaonekana kama zezeta.
“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa kuamkia
leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana
mlango...wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo
ndani na usiku alipewa chakula akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu
wa karibu wa mwanamke huyo.
Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa
kienyeji amekwisha kuja kwa ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze
kurudia hali yake na kwamba amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka
maiti kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alithibitisha tukio hilo,
lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za kishirikina.
Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika eneo la tukio
kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni jana, maiti ya
mwanamke huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.
Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.
Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe Ngitu Masisanga na mama yake
mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua ghafla juzi baada ya
kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
Alisema cha ajabu ni kwamba wakati wamelala nyumbani kwa marehemu
sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku marehemu alitokea akiwa
uchi.
Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na kutazama picha hizo na
kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo alichukua tochi iliyokuwa
ikiwaka na kuizima.
Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya
kukimbia nje tulimzuia yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio
tukakimbilia nje, licha ya kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu
ufunguke ila na yeye aweze kutoka nje, kuna mtu amefanya dawa za
kienyeji ndio tunasubiri majibu.”
No comments:
Post a Comment