Na Luqman Maloto
MISS
Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kabla ya mwaka 2010, alishahusishwa
kimapenzi na wanaume kadhaa, akiwemo Khaleed Mohamed ‘TID’, Hery Samir
‘Mr. Blu’, Jack Pemba, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’, Hartmann Mbilinyi,
Jumbe Yusuf, marehem Steven Kanumba ‘The Great’ na wengineo.
Mtoto mduchu anayefanya Bongo Fleva, Nasib Abdu Juma ‘Diamond’,
alianza kung’ara mwaka 2010 pale aliponyakua tuzo tatu za Kili Music
Awards na baada ya hapo, alijihesabu kuwa staa,hivyo kula sahani moja na mastaa ambapo sasa matokeo yanaelekea kumfelisha kimuziki.
Jumamosi
iliyopita, Diamond alifanya shoo kwenye Fainali za Miss Tanzania
2012-2013 na jinsi alivyoonesha uwezo mdogo siku hiyo, wadau walinena
kwamba kijana ameanza kufeli kimuziki, ule uhodari wake wa kucheza na
jukwaa umepotea.
Diamond akipondwa na kushushwa hadhi, nyuma yake
kuna maneno kuwa chanzo cha uwezo wa dogo huyo kushuka ni mapenzi na
mhusika mkuu ni Wema. Ipo wazi kwamba Diamond na Wema wameshindwa
kuachana licha ya kutangaza kufanya hivyo mara nyingi.
HUU NDIYO MWANZO WA MWISHO WA DIAMOND?
Mwanzo
wa mwisho ni msemo kutoka kwenye maneno ya Kiingereza, The beginning of
the end. Hoja ni kwamba kiwango kidogo alichokionesha Diamond kwenye
jukwaa la Miss Tanzania ni ashirio baya kuwa huenda ndiyo mwanzo wa
mwisho wake kutamba kimuziki.
Kilichoonekana siku hiyo ni kwamba
Diamond hana jipya na zaidi ameanza kuwa mzito jukwaani. Amekosa ubinifu
wa kumfanya shabiki amuone wa tofauti. Amebaki yuleyule, hivyo biashara
yake inaelekea ukingoni.
Kwa macho rahisi unaweza kutoa kauli kwamba
Diamond amebweteka au amelewa sifa lakini ukweli ubaki kwenye mstari
kwake kuwa penzi la Wema ni kilevi kikali kwake ambacho kwa kasi ya
ajabu kinampotezea dira.
Diamond baada ya kulewa mapenzi ya Wema,
sasa amegeuka sokomoko au pampula. Na kwa sababu ‘bwa mdogo’ huyo asili
yake ni Kigoma, kule mlevi huitwa mboregwa, kwa hiyo binti wa Balozi
Isaac Sepetu, amemfanya staa wa wimbo wa Mbagala awe mboregwa wa
mapenzi.
Kama zamani alipokuwa anafanya shoo, watu walikuwa hawakai,
wanacheza na kumiminika jukwaani kumtuza, siku hiyo aliimba wapi!
Akateremka kuwafuata mashabiki walipo lakini hakuna aliyesimama wala
kuonesha kusisimkwa na shoo yake. Napigia mstari, this is the beginning
of the Diamond’s end.
Hivi karibuni katika shoo ya Fiesta 2012,
Diamond alishindwa kupokea shangwe zilizozoeleka, hata alipoamua kuvua
nguo na kubakisha ile ya ndani, bado alichemka. Zaidi akaonekana
kuharibu zaidi kuliko kujenga.
Diamond alivua nguo, kipindi ambacho
Wema yupo kwenye gumzo zito kutokana na jinsi ambavyo alikuwa anacheza
nusu uchi jukwaani katika shoo kadhaa za Fiesta 2012. Kwa maana hiyo,
Diamond alipovua nguo ilitafsiriwa amemuiga Wema.
Unapomuiga mtu
maana yake unakuwa umemkubali, kwa hiyo Diamond ‘amechizika’ kwa Wema
kiasi ambacho hata uchafu anaoufanya yeye anauiga. Kwa mantiki hiyo
Diamond na Wema ni kama boyfriend kama girlfriend (like a boyfriend like
a girlfriend).
DIAMOND ANAHARIBIKA SI UTANI
Hapati
muda wa kufanya mazoezi, anatumia muda mwingi kujiuguza maradhi ya
mapenzi. Hii ndiyo sababu kwamba sikushangaa kumuona akichemka jukwaani.
Wala sijiulizi ni kwa nini kiwango chake kinaporomoka kwa kasi.
Oktoba
26, 2012 usiku wa kati ya saa 8 na 9, nikiwa naendesha ‘kibebi-woka’
changu nikitokea ofisini kwetu Bamaga, Mwenge, naelekea nyumbani
Kijitonyama, nilipofika Mtaa wa Akachube (Kijitonyama), nilimkuta Wema
akiwa anaongea na simu huku amezungukwa na watu.
Nikafunga breki,
nikashusha kioo nikamsalimia naye akaitika. Nilipoona hayupo kwenye hali
ya kawaida nikashuka. Stori niliyoipata pale ni kuwa kumbe alikuwa
amegombana na Diamond muda mfupi uliopita.
Eneo la tukio (jirani
kabisa na kwa Wema), alikuwepo pia mwanamuziki Omar Faraji Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’. Nilipoona mazingira hayavutii, nikamuacha Ommy anamtuliza Wema,
mimi nikaondoka zangu.
Asubuhi nikaambiwa kuwa Diamond alirudi
nyumbani kwa Wema, suluhu ikapatikana. Jaribu kufikiri kuwa kama mtu
usiku wa manane yupo bize na mapenzi, migogoro isiyokwisha ni saa ngapi
atatulia kubuni shoo? Ni muda gani atautenga kwa ajili ya kutengeneza
staili mpya?
JE, ANAYAJUA YALIYOMKUTA KANUMBA KWA WEMA?
Mungu
amlaze mahali pema marehemu Kanumba ambaye ndiye aliyemfanya Wema
aingie kwenye ulimwengu wa filamu. Mapenzi yalipokolea, The Great
alilewa kiasi kwamba alishindwa kabisa kustahimili vishindo.
Kwa mara
ya kwanza Kanumba aliripotiwa kupigana kwa sababu ya Wema. Staa huyo wa
filamu akawa hatulii, mara yupo polisi kwa sababu ya kesi ya Wema,
ufanisi wake ukaporomoka. Nadhani kuna kitu, sasa namuona Diamond
anashika mkondo uleule.
Kanumba aliposhtuka alimuacha Wema na kuanzia hapo alirudi kung’ara kwenye soko la filamu.
Wema
alimchonganisha Kanumba na Jumbe wakapigana, mwanamke huyo
kawachonganisha Diamond na hasimu wake, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’.
Ikidaiwa kuwa mrembo huyo amempa penzi Bob Junior.
No comments:
Post a Comment