Mwalimu ni kiungo muhimu sana katika malezi ya wanafunzi hapa nchini.Wao hushinda na watoto wetu kutwa nzima .......
Kwa mantiki hiyo, tabia ya mtoto yeyote aliyewahi kalia madawati ina asilimia zaidi ya 70 ya tabia za walimu wake......
Siku hizi mambo yamebadilika sana.Mwalimu wa miaka ya 90 ni tofauti kabisa na mwalimu wa miaka y leo.
Walimu wa leo wengi wao ni vijana wadogo
ambao wengi wamejawa na tamaa za mapenzi.Wao hawajui kutongoza bali
wanajua kulazimisha....
Inashangaza na kusikitisha kuona walimu wetu wakishindana KUTOA BIKRA ZA WATOTO WA KIKE......Mtoto akikataa basi cha motoatakiona ....
Mtandao huu umebahatika kuongea na
mwanafunzi mmojaambaye ni mhanga wa tukio hilo la kulazimishwa mapenzi
na mwalimu wake..........
HILI NI SIMULIZI LAKE:
--------------------------------------------------------------------
"Mwalimu alianza kunitaka tangu
nikuwa form one.Nilipomkataa alianza kunichapa tena bila kosa maalumu
na kunipa adhabu kila mara...
Baada ya kufanya hivyo kwa muda,
aliamua kuniita ofisini na kuniambia kuwa anatanisaidia kimasomo
endapo ntamkubalia.Niliamua kumkubali kwa kwa kuhofia viboko na
aliniambia nisimwambie mtu.
Siku ya kwanza kufanya mapenzi
alinipeleka gesti na aliniambia kuwa atatumia condom.Kwa kuwa ilikuwa
ni mara yangu ya kwanza hatukuweza kutumia kinga na alifanya
hivyohivyo.
Baada ya hapo tuliendelea kufanya
hicho kitendo hata tukiwa shule.Wakati wa kutawanyika, mwalimu alikuwa
akiniita katika ofisi yake na kunilazimisha tufanye.....
Miezi kadhaa baadaye, nilianza
kujihisi tofauti na wazazi wangu waliyagundua mabadiliko
hayo.Walinipeleka hospitali na vipimo vilionesha kuwa nna
mimba.Waliponibana ilinibidi niwaeleze ukweli.....
AFISA ELIMU AINGILIA KATI:
Baada ya kubaini hali hiyo, baba
alinipeleka moja kwa moja mpaka kwa afisa elimu wa mkoa.Sikuwa na jinsi
zaidi ya kueleza ukweli.Mwalimu aliitwa na kuhojiwa.Mwanzo alikataa
kabisa lakini baada ya kubanwa ilibidi akubali.
Mwalimu alisimamishwa kazi kwa muda
na kufunguliwa mashitaka.Alikaa polisi kwa siku mbili, siku ya tatu
alipata dhamana akatoka.....
Alipotoka, mwalimu aliamua kujiua kwa sumu.Shule niliachishwa.nipo nyumbani na mtoto.
--------------------------------------------------------------------
MTAZAMO WETU:
Ni ukweli usiopingika kuwa walimu wa
siku hizi wamekuwa ni kero kwa watoto wa kike.Walimu hao hutumia
viboko kama msingi wa kuwafanya wakubaliwe maombi yao.Hii ni
changamoto kubwa sana inayotukabili sisi wazazi.
Nadhani huu ni wakati mwafaka kwa
wanafuni kujitambua na kutokuwa wasiri kwa kuhofia kuchapwa
viboko.Waeleze wazazi wako juu ya mkasa unaokukabili maana hayo ndo
maisha yako ya baadaye
No comments:
Post a Comment