Akinukuliwa na mtandao huu, ua hili limesema kuwa lina hasira ya muziki na kuwa pwani hii haina mwanamuziki mwengine wa kike mwenye sifa zaidi ya Nyota Ndogo.
( R-zee katika pozi la picha........)
R-zee ambaye ashawahi kushirikiana na wanamuziki kama vile Cld, Crazy P na wengine wengi, adokeza kuwa ipo haja ya majumba ya habari kuwapenda wanamuziki wa kike hapa pwani na pia kuufagilia muziki wao.wakati uo huo, mrembo huyu hakuachwa nyuma kuwapa vijembe warembo wenzake walio katika ulingo huu wa muziki kuwa ni lazima wajiheshimu na wafanye kazi za maana pasi kujiachilia kwa majina makubwa na kisha kudororeshwa kimziki.
(kama Mfb twamtakia kilala heri.....)
No comments:
Post a Comment