Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini Joseph Haule a.k.a Prof. Jiize ambaye hivi karibuni amefungua studio yake inayokwenda kwa jina la Mwanalizombe iliyopo maeneo ya Msasani mwisho ambayo hadi sasa tayari JCB ameshaingia lebo kwenye studio hiyo.
Ikiwa ni kawaida kwa kila studio kuwa na mikakati yake juu ya kuwasaidia wasanii wachanga ili waweze kutoka na kuendelea kimuziki, Jay mbali na kuwasaidia lakini ametoa angalizo juu ya artists wapya wote ambao wanatarajia kuingia kwenye muziki au tayari wapo kwenye gemu na hawajasimama sawa sawa.
“Labda niseme kitu kimoja kwamba mwanzoni watu wa rika zote waliupenda muziki wetu kwa dhati na ikafika kipindi waliamua kuwekeza kwenye muziki kwakuwa mashairi yalikuwa yanafundisha,kuelimisha, kuburudisha,kukosoa na kusifia inapobidi na yote haya yalifanyika ili kuieleza jamii kwamba dhana ya muziki sio uhuni ndio maana wasanii walijitahidi kutoa nyimbo zenye ujumbe,tofauti tofauti kwa jamii.” – Prof. Jay.
“Sasa basi ili hawa vijana wanaochipukia kwenye huu muziki wetu lazima waangalie mbali sana ili kuzidi kuilinda hadhi ya mziki wetu ambayo haikuwa rahisi kuitafuta na kuisimamisha hadi kufikia watu kuiamini Bongo Fleva kama moja kati ya aina ya mziki yenye mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kuondoa vijana wengi vijiweni bila ajira na kuwapa ajira ya kudumu na hata kuishi maisha ya ndoto zao za zamani. Kikubwa ni heshima ya kazi na juhudi ka kwanza ndipo fedha itakuja na kuitumia utakavyo.” – Prof. Jay.
No comments:
Post a Comment