MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul,
anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya
watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa
hivi karibuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions,
Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo
katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.
“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao
wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki
kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na
wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu
na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.
Akizungumzia kuhusu video hiyo, Mwendapole alisema
itarekodi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo
msanii huyo analiangalia kwa sasa huku video hiyo ikifanya na kampuni bora
kabisa Tanzania.
Kwa upande wake Diamond alisema lengo kubwa la
kufanya hivyo ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muziki nchini lakini pia
kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana ambao wako mitaani lakini
wanapenda muziki.
Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani wiki
iliyopita anatarajiwa tena kwenda Marekani kwa ajili ya onyesho moja la muziki.
Msanii huyo alifanya mapinduzi katika medani ya
muziki wa bongo baada ya kufanya onyesho lake alilolipa jina la Diamond’s are
Forever pale Mlimani City ambapo katika shoo hiyo aliifanya mwenyewe na
kiingilio kikiwa sh 50,000 jambo ambalo halijawahi kufanyika katika ulimwengu
wa muziki nchini.
No comments:
Post a Comment