flash3

Friday 6 December 2013

DAZLAH_ILLUMINATI?????

(Dazla Kiduche Katika Poz.)
Msanii Mkali Kutoka Pwani Ya Kenya Dazla Kiduche Anatarajiwa Kushangaza Wengi Baada Ya Kukosa Kufunguka Kinaga Naga Kuhusu Swala Zima Linalo Tamba La Illuminati.
Akihojiwa Na Tafrija Select Pwani Fm, Kiduche Alidinda Kufunguka Wazi Huku Akisema Kuwa Haamini Illuminati Na Mambo Yao Japo Anafahamu Kuwa Wapo Aidha Kiduche Kafunguka Akidai Kuwa Mungu Ndio Nira Yake Ya Ushindi Maishani.
Swala La lIluminati Limehusisha Wasanii Wengi Hapa Pwani Wanaoonekana Wakishamari, Wakiwemo Susumila Na Kidis, Swala Walilolipuuza Kama Uvumi Wa Chuki Kwani Fani Hii Inao Uwezo Mkubwa Wa Kukidhi Walicho Nacho Na Wanachokihitaji Katika Maisha Yao.
Dazla Mkali Wa Vibao, Mapenzi Nyara, Mlevi Wa Mapenzi Na Inawauma Aliomshirikisha Kidis The Jembe, Asema analenga Kuitaabisha Anga Na Talanta Yake Bila Kuwakosesha Utamu Mashabiki Wake.
Mkali Huyu Aliongezea Kusema Kuwa, Hana Ushindani Na Mtu Wala Watu Bali Yupo Mbioni Kushindana Na Kile Ambacho Mungu Alimpa, Huku Akisisitiza Kuwa Kile Mungu Alimpa Hajakifikia.
Kuhusu Swala La Mkataba Wake Na Can Candy Kiduche Hakutaka Kulizungumzi wala Hilo Ikizingatiwa Kuwa Kumekuwa Na Msuko Suko Baina Yake Na Kandarasi Yake Uongozi Wa Kampuni Hiyo.
Mfb Ina Mtakia Kiduche Kilala Heri.

No comments:

Post a Comment