flash3

Tuesday 26 February 2013

HII NDIO PETE LINEX AMEMVISHA MCHUMBA WAKE

Weekend hii, mtu mzima Sunday Mjeda aka Linex aka Mr VOA (Voice Of Africa), alifanya yake kwa kumvisha pete mpenzi wake, ambae ni  mwenyeji wa Finland anaeitwa Suvi. Linex aliamua kufanya kimya kimya tena wakiwa wawili tu, kwasababu hakutaka kujionyesha, na anaamini ile ni kitu very personal haikuhitaji manjonjo mengi...all in all blog hii inakutakia kila la kheri
 



 

Wednesday 20 February 2013

WEMA ATAMBULISHA RASMI OFISI YAKE MPYA "ENDLESS FAME FILM"

 Siku chache baada ya msanii wa tasnia ya filamu Bongo, Wema Abrahamu Sepetu kutangaza kuwa anamiliki kampuni mpya ya filamu"Endless Fame Film" leo mchana aliweza kufanya press conference na waandishi mbalimbali huku akitambulisha rasmi kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa msanii huyu alisema kwamba kwasasa bado ofisi yake haijaanza kufanya kazi ila inatarajia rasmi kuanza kazi mwezi wa tatu mwaka huu.@Wema alisema....

    Tazama picha za ofisi yake mpya 'Endless Fame Film' iliyoitambulisha leo rasmi.......











                                                               Wema na Zamaradi
                                                                  Wema na Dotnata
                                                                     Wema na Rich
                                                                        Cloud na JB 

Tuesday 19 February 2013

LINEX AMTANGAZA RASMI STARA THOMAS KUJIUNGA V.O.A

Linex Sunday baada ya kuunda kundi lake jipya linalofahamika kwa jina la Voice of African na kupelekea mashabiki wengi kukubali kazi zao katika tasnia hii.
Leo kupitia katika ukurasa wa linex aliandika"Nachukua nafasi hii kumtangaza mwana dada Mwenye sauti ya tofauti Stara THomas kuanzia leo atakua ni mwanamuziki kutoka V.O.A kama una swali kuhusu hili litajibiwa"alisema Linex
Kwa hiyo wale mashabiki wa Voice of Africa kuanzia sasa utakuwa ukimsikia Stara Thomas ndani ya Kundi ilo

Friday 15 February 2013

REST IN PEACE GOLDIE HARVEY

Kupitia mitandao ya Nigeria inaendelea kusikitika kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Nigeria katika shindano la Big Brother Afrika 2012,Goldie harvey, na mchumba wa rapa kutoka Kenya Prezzo.
Habari zinaendelea kupokelewa kwa hisia tofauti huku wengine wakiwa bado hawaamini kama kweli Goldie amefariki lakini ukweli ni kwamba mitandao yote ya nchini Nigeira iimedhibitisha kifo hicho.

Hii ni taarifa rasmi kutoka katika label yake Kennis Music  kuhusiana na kifo chake.
kwa niaba ya Kennis Music, nasikitika kuthibitisha rasmi kifo cha ghafla na kushtua cha pop satr wa Nigeria Goldie Harvey.

"Goldie, 31, amefariki alhamis baada ya kulalamika kupatwa na maumivu makali ya kichwa katika jumba lake lililopo park view, muda mfupi baada ya kurejea kutoka marekalani, alipoenda kushuhudia tuzo za Grammy. aliwahishwa katika hospitali anayotibiwa Reddington, Victoria Island, Lagos, ambapo madactari walisema amefariki baada tu ya kufika".

mwili wa marehem Goldie, umeshapelekwa katika mochuari  ya Lagos University Teaching Hospital iliyoko Ikeja, Lagos. Goldie aliiwakilisha Nigeria katika  Big Brother Star Game 2012.

Juhudi zake za  hivi karibuni, ni pamoja na single tatu kutoka katika album yake ya nne iliyokuwa inafata "African Invasion", "skibo", "Miliki" na "Got to have it" ambazo kwa sasa zinapata kuchezwa sana katika vituo mbali mbali vya redio na tv Africa.

Mipango ya mazishi itatangazwa na familia yake.."

Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi, Amen

Hii ni video ya ngoma aliyoshirikishwa na Ambwene Yessaya 'Skibobo'

Thursday 14 February 2013

JB AZUSHIWA KIFO


Msanii nguli wa maigizo nchini Tanzania Jacob Stephen maarufu “JB” jana alikumbwa na wakati mgumu baada ya kuzushiwa kwamba amefarki dunia.Story hiyo ilimshutua sana msanii huyo, baada ya kupokea simu nyingi lakini haikumstua kwani alishapigiwa simu kupewa taarifa ya msiba wa mmiliki wa hoteli za JB Belmont Bwana Justice Baguma “JB”.

Akizungumza na Movie leo ya Leo Tena ya Clouds FM, JB amesema alishtushwa sana na taarifa hizo.
“Nilipata mshtuko nilipaonza kupata simu nyingi sana kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki kuniuliza hali yangu lakini ilikuwa rahisi kuwaelezea watu coz nilikuwa aware kuhusu mtu aliyefariki na hii iliisha baada ya simu yangu kuisha charge kutokana na kupokea simu nyingi sana.”
JB ameongeza kuwa “Mimi bado naendelea kusurvive na niko sawa kabisa ila nawapa pole sana watu wangu wa karibu kwa mshtuko waliopata pia ndugu jamaa na marafiki wa marehemu JB Belmont nawapa pole sana ila napenda watu wakumbuke kuwa jina langu halisi ni Jacob Stephen hiyo JB ni inital tu”

MOURINHO: HATUWEZI KUTOKA KAPA OLD TRAFORD




Mourinho ana amini kwamba Real Madrid watafunga goal zaidi ya moja watakapo kutana tena na Manchester United huko Old Trafford.
Mourinho aliwaeleza sky sports kwamba “Wachezaji wangu wametoa kila walichokuwa nacho, mchezo huu ulikuwa mgumu na nisingeweza kukubali kufungwa 1-0. Ni wakati wetu sasa kwenda old trafford, 1-1 sio matokeo mabaya tunaamini kuwa tunaweza kufunga goal zaidi ya moja huko old trafford”

“Walipata nafasi mbili nzuri kipindi cha pili lakini nafasi hizo hazina maana sana kwamaana sisi ndio tulimiliki mpira sana. Hii ni ligi ya mabingwa, ni mechi mbili nyumbani na ugenini. Mechi yao wamefanya vizuri.

Wednesday 13 February 2013

MSANII WA KUNDI LA WANAUME HALISI AFARIK8I DUNIA

Msanii na mmoja wa waasisi  wa kundi la Wanaume Halisi Baraka Masale au "BK"  Pichani amefariki Dunia leo katika hospitali ya Muhimbili. BK alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo kwa muda mrefu. Mungu ailaze mahala pema peponi Roho ya Marehemu.
Leo alfajiri game ya muziki wa kizazi kipya imempoteza nyota wake ambaye alikua member wa kundi la TMK Wanaume halisi.The late Baraka Sekela, kwa jina la stage ni BK, ambaye yeye ni moja kati ya waasisi wa kundi la TMK Family, hata makao makuu ya kundi hilo yalikua nyumbani kwa wazazi wake karibu na uwanja wa taifa wilaya ya Temeke, jijini dar es salaam.
Marehemu bk alikua anaumwa, hadi mauti yanamkuta alikua amelazwa hospitali ya rufaa ya muhimbili.
"Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu sana Hassan Omandi, marehem alikua anaumwa tumbo kwa takribani siku tisa na kuambiwa ana taifod katika hospitali aliyoenda kufanya vipimo, lakini baada ya kuanza dozi akazidiwa kabisa, ikabidi twende hospitali ya Temeke, kule wakaona ni tatizo kubwa na kumpeleka Muhimbili, ndio huko akaambiwa ini lake linamatatizo ya kuvimba."amesema rafiki yake wa karibu anaeitwa Hassan Omande

KIGOMA ALL STARS WALA SHAVU LA KUWA MABALOZI WA NSSF

#InstaConference #Arusha #AICCR #AsNSSFFambassador #KiCorporateZaidi #KiNSSFzaidi #Mipango na #MaendeleoZaidi #kiCommunity na #Member wenzangu toka #LekaDutigiteCompany
Leo hii ikiwa ni dakika 30 zilizopita, kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na Banana , Mwasiti na wengineo wanaounda kundi la Kigoma All Stars, wakiwa  katika ukumbi wa mikutano Arusha AICC. Kutokana na maelezo aliyoyaandika chini ya picha hii, ni dhahiri kuwa wamekula shavu la kuwa mabalozi wa NSSF.
Kama unakumbuka siku chache zilizopita, tulikuwekea picha hii ya tangazo la NSSF likiwa na picha ya wasanii hao ya wasanii hao

Thursday 7 February 2013

AFANDE SELE AMPA UFALME ROMA


Legend wa Hip Hop Music Tzee Afande Sele ambaye jina lake halisi ni Selemani Msindi amemvulia kofia msanii anayetisha kwa sasa katika gem Roma Mkatoliki akidai ndie ”mfalme” kwa sasa kwa umahiri wa kuandika mistari yake.
Afande amefunguka kuwa

ukali wa rapa huyo unampa hope kubwa ya kuhisi kwamba wamepatikana warithi wa kuendelea Hip Hop Tzee akimpa sifa kabambe kwa kuwa na uwezo mkbwa wa kutunga mistari ya ngoma zake.
Mkali huyo wa Hip hop kutoka Morogoro amefafanua kuwa katika muziki wa kizazi kipya kuna usaliti mkubwa hali ambayo inamfanya sasa kuamua kupumzika kwa muda na kujikita kwenye masuala ya filamu.

Tuesday 5 February 2013

Kali Zetu...


PREZZO KUFUNGA NDOA NA GOLDIE FEBRUARY 9

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini Nigeria, rapper Jackson Makini maarufu kama Prezzo, anatarajia rasmi kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.
Baada ya taarifa hiyo kuendelea kuenea katika mitandao pia inasemakana kwamba harusi hiyo itafanyika jijini Lagos nchini Nigeria.

Q CHIEF NDANI YA BBA????

 Kutoka 255 ya xxl ya Clouds Fm, mtu mzima Q chief, amehabarisha hatua aliyoichukua leo hii, kuelekea katika office za MultChoice zilizopo barabara ya Ally Hassan Mwinyi, na kuchukua form kwa ajili ya usahili wa kumpata muwakilishi atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo mwaka 2013.Qchief amekua ni mtu maarufu wa pili kuchukua form baada ya mwanadada Wema Sepetu kuchukua form wiki iliyopita

Friday 1 February 2013

WEMA SEPETU ACHUKUA FOMU KUSHIRIKI BBA 2013

 
Muigizaji Wema Sepetu, leo hii ametia tim offisi za Multchoice na kuchukua form kwa ajili ya kushiriki kwenye mchakato wa kwanza wa shindano la Big Brother  Africa BBA, 2013