flash3

Thursday 14 February 2013

JB AZUSHIWA KIFO


Msanii nguli wa maigizo nchini Tanzania Jacob Stephen maarufu “JB” jana alikumbwa na wakati mgumu baada ya kuzushiwa kwamba amefarki dunia.Story hiyo ilimshutua sana msanii huyo, baada ya kupokea simu nyingi lakini haikumstua kwani alishapigiwa simu kupewa taarifa ya msiba wa mmiliki wa hoteli za JB Belmont Bwana Justice Baguma “JB”.

Akizungumza na Movie leo ya Leo Tena ya Clouds FM, JB amesema alishtushwa sana na taarifa hizo.
“Nilipata mshtuko nilipaonza kupata simu nyingi sana kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki kuniuliza hali yangu lakini ilikuwa rahisi kuwaelezea watu coz nilikuwa aware kuhusu mtu aliyefariki na hii iliisha baada ya simu yangu kuisha charge kutokana na kupokea simu nyingi sana.”
JB ameongeza kuwa “Mimi bado naendelea kusurvive na niko sawa kabisa ila nawapa pole sana watu wangu wa karibu kwa mshtuko waliopata pia ndugu jamaa na marafiki wa marehemu JB Belmont nawapa pole sana ila napenda watu wakumbuke kuwa jina langu halisi ni Jacob Stephen hiyo JB ni inital tu”

No comments:

Post a Comment