flash3

Monday 7 May 2012

DIAMOND ATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA YATIMA

 ICON katika mziki wa Bongofleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ jana alitoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre ambacho mwanamuziki TID anadaiwa kula fedha za yatima wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Kinondoni Hananasif jijini Dar.

Akizungumza na mtandao huu kabla hajakabidhi msaada huo, Diamond alisema kuwa kikubwa zaidi kilichomfanya hadi atoe msaada huo ni kuguswa na maisha wanaoishi  yatima hao.
“Unajua siku zote Mungu anasema unachokipata ugawane na wenzako, sasa mimi pamoja na meneja wangu Joffrey a.k.a Joff tumeona tutoe nusu ya kile tulichokipata  kwa hawa ndugu zetu wanaolelewa katika kituo hiki,” alisema Diamond.…

No comments:

Post a Comment