flash3

Monday 7 May 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LULU......

 Lulu (katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa k***.

Huku kesi ya inayomhusu Msanii wa filamu za maigizo nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’, jana alipandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.

 hatima yake ni gani mwana dada ,huyu jamani?

No comments:

Post a Comment