flash3

Tuesday 7 July 2015

Selfie Hiyoooo! ikazua darajani Huko Kwa Warusi........

Upigaji wa picha za selfie bado umeendelea kupata umaarufu katika sehemu mbalimbali duniani kutokana na teknolojia ya mitandao ya kijamii kuendelea kukua kwa kasi.
Matukio ya watu kupoteza maisha wakati wakitaka kupiga selfie za kipekee imekua ikitokea kila wakati lakini watumiaji bado wanashindwa kuwa makini.
Stori ya leo inatokea huko Russia ambapo msichana mmoja amepoteza maisha wakati akipiga selfie na wenzake juu ya daraja maarufu lililopo eneo la  Moscow International Business Center.
Uchunguzi wa polisi umesema tukio hilo lilitokea siku ya jumamosi ambapo msichana huyo akiwa na rafiki zake walianza kupiga picha juu ya daraja hilo bila kuchukua tahadhari na ndipo upande wa daraja hilo ulikatika na mmoja wao kudondoka na kupoteza maisha.

No comments:

Post a Comment