flash3

Wednesday 8 June 2016

NI RASMI TIWA SAVAGE ASAINIWA NA JAY Z NA SASA ATAKUWA CHINI YA ROCK NATION (@tiwasavage)


Jana imekuwa Rasmi Jay Z amemchukua msanii wa Kwanza Kutoka Africa Kumsimamia Kupitia Rock Nation ambaye si mwingine bali ni Hit Maker huyo wa Eminando, Tiwa Savage.
Tiwa Ametuthibitishia kupitia Account yake ya Instagram kwa kupost Picha akiwa na Jay Z Pamoja na C.E.O wa Mavins Records Don Jazzy katika Office za Rock Nation New York Marekani na kuipa Caption Mavin X Roc Nation 🙏🏽 hii ikimaanisha kwamba Tiwa Atakuwa chini ya Label Hizo 2 yaani Mavins kwa Uapnde wa Kuikaba Africa na Rock Nation kulikaba soko la Dunia.

Wakati Najaribu kufikiria Jinsi ambavyo Mumewe Teebillz Ambaye wameachana Majuzi anavyojiskia Nataka nikupe List ya Wasanii ambao Wako chini ya Rock Nation.
Wasanii wanaofanya kazi chini ya Rock Nation ya Jay Z ni: Jay Z Mwenyewe, Rihanna, Dj Khaled, Dj Mustard, Jay Cole, DJ Khaled , Jay Electronica, Willow, Romans, Big Sean, na wengine.
Nawaza Pia kama Teebillz alisema Mkewe Tiwa Savage anatoka na Don Jazzy, Sasa hivi si ndo atazimia Kabisa sababu watakuwa wanakula sana Upepo wa Angani na Hotel kubwa za Marekani Wakiwa Pamoja.
Hongera sana kwa Tiwa Savage kwa Kula Shavu kubwa na huu uwe Mfano mzuri kwa Wasanii wengine wa Africa haswa wa Kike na Naamini Ubalozi wake na Makampuni kama Pepsi, Forte Oil, na MTN utaongezewa Unono zaidi.

No comments:

Post a Comment