flash3

Thursday 9 May 2013

CHRIS BROWN AKERA MAJIRANI

chris brown
Chris Brown ambaye kila kukicha amekuwa mtu wa matukio mapya, ametokelezea na mpya nyingine tena hasa baada ya majirani zake huko Hollywood Hills kuendelea kuwa ni changamoto kwake, na safari hii wakiwa na malalamiko makubwa juu ya graffitti ambazo msanii huyu amezichora katika eneo hilo.
Hii imekuwa si changamoto pekee katika hili hasa kutokana na malalamiko mengine mengi kuhusiana na sauti kubwa ya muziki kutoka kwenye nyumba ya msanii huyu ambapo tayari amekwishapatiwa maonyo kadhaa kujirekebisha kama anataka kuepukana na adhabu pamoja na faini.
Msanii huyu pia kwa upande mwingine, amepamba vichwa vya habari baada ya kuzungumza katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kuwa mahusiano yake ya kimapenzi na Rihanna yamekwisha hasa kutokana na tofauti zao pamoja na umri wao mdogo kwa sasa.

No comments:

Post a Comment