flash3

Thursday 9 May 2013

REDSAN AGHARAMIA KIDEO

redsan
Ili kudhihirisha kuwa amejipanga na hatanii katika kazi zake, Msanii wa muziki wa mindoko ya Dancehall kutoka humu nchini, Redsan amesema kuwa, Video ya ngoma yake mpya ya Badder Than Most, itafanyiwa shooting kwa sehemu nchini Kenya, na kwa sehemu nyingine itafanyika huko Miami.
Redsan amesema kuwa hatua hii ni kwa ajili ya kuipatia video hii muonekano halisia wa kujiachia na kupati, na amejipanga sawa sawa kuhakikisha kuwa hili linafanyika kwa ubora wake.
Hatua hii ambayo amejipanga kuifanya Redsan ni ya gharama kubwa kiasi chake ingawa msanii huyu amekataa kabisa kutaja fungu ambalo ameliandaa kukamilisha kazi hii, na sasa macho ya wapenzi wengi wa muziki yanasubiri kuona video yenyewe itakuwaje.

No comments:

Post a Comment