flash3

Wednesday 8 May 2013

WIZKID APASUA ANGA

Wizkid
Akiwa bado anamake headlines nchini Nigeria rapa Wizkid anazidi kudhihirisha kuwa anaimudu game ya muziki na hivi sasa mkali huyo amefyatua wimbo mpya alioufanya na mwanamuziki nguli wa miondoko ya Afrobeat na mshindi wa tuzo maarufu za grammy barani Afrika, Femi Kuti katika wimbo uliobatizwa jina, (SHEIYO SHEIYO)
Ayo Balogun aka Wizkid ambaye hivi karibuni alisaini upya mkataba wake na label ya EME, ametoa trak hiyo mpya na nyota huyo ambaye ameupamba wimbo huo kwa utaalamu wake wa kutumia chombo cha muziki aina ya saxophone.
Trak hiyo imefanyiwa utayarishaji na Prodyuza Sarz ambapo Wizkid mwenyewe ameelezea kuwa mnamo tarehe 12 mwezi June mwaka huu anatarajia kuachia albamu yake chini ya label za EME na Starboy Entertainment act.

No comments:

Post a Comment