flash3

Wednesday 8 May 2013

PAUL P.SQUARE ADAIWA KUTELEKEZA MKE

Paul okoye
Imeelezwa kuwa nyota wa kundi maarufu la P Square nchini Nigeria, Paul Okoye amemtelekeza mama wa mtoto wa pili wa nyota huyo katika hospitali moja jijini London nchini Uingereza ambako mwanamama huyo amejifungua mtoto wake wa kiume anayesemekana amebatizwa jina la Michelle Paul Okoye.
Habari hizo ambazo zimesambaa kupitia mitandaoni na kushtua mashabiki zimeelezea kuwa zimepita wiki kadhaa nyota huyo kuzaa mtoto wake wa kwanza huko Atlanta na aliyewahi kuwa mlimbwende mmoja ambaye Paul amekataa kuchukua jukumu la kumlea mtoto huyo wa kiume.
Hivi sasa mama huyo ambaye Paul amemtelekeza huko London anajulikana kwa jina la Elshama Benson Igbanoi, mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mlimbwende wa jimbo la Plateau, aliyejifungua huko Queen Charlotte katika hospitali ya Chelsea London.
Taarifa zilizopo ni kuwa hospitali hiyo inamdai mwanamama huyo gharama za kujifungua na matibabu yanayofikia kiasi cha paundi elfu tano.

No comments:

Post a Comment