flash3

Wednesday 8 May 2013

LAURYN HILL KWENDA JELA

LAURYN HILL
Baada ya kufeli kulipa deni la kodi la dola milioni 1 ndani ya wakati aliokuwa amepewa na mahakama, Mwanamuziki mkongwe mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Grammys, Lauryn Hill amehukumiwa kifungo cha miezi 3 jela.
Mbali na kukomaa na kulipa kiasi cha dola laki 9, zaidi ya shilingi bilioni 1 na milioni 400 za kitanzania mpaka juzi, ili kujaribu kujiokoa na kitanzi hiki, Deni la mwanadada huyu bado lilionekana waziwazi kumuelemea hasa kutokana na riba na faini ambazo ziliongezeka katika madeni yake ya muda mrefu.
Hill kwa sasa anajipanga kujirudisha tena katika game ya muziki na kwa mujibu wa hukumu anatakiwa kuripoti gerezani tarehe 8 mwezi July kwaajili ya kuanza kutumikia kifungo chake.

No comments:

Post a Comment