flash3

Wednesday 5 December 2012

MFANYABIASHARA WA KIKE KUTOKA HUMU NCHINI KENYA AJIUA KWA UPWEKE UINGEREZA

 
Sharon Bukokhe enzi za uhai wake.
 
Sharon Bukokhe akiwa kajipumzisha nyumbani kwake.
MREMBO Sharon Bukokhe, 28,  Mkenya aliyehamia Uingereza, amejiua kwa kujikuta akiishi katika upweke wakati familia yake imetawanyika sehemu mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na vyombo husika, Bukokhe alijiua mwezi Aprili nyumbani kwake kutokana na familia yake kuwa mbali naye, akiwemo mumewe ambaye yuko Afrika Kusini.
                                                Sharon kabla hajaamua kuitoa roho yake.
Ujumbe aliouacha nyumbani kwake kabla ya kujiua ulisema: “Nafikiri maisha yangu ni ya thamani kama yajayo, kwa vile kufa ukiwa na umri wa miaka 25 ni sawa na kufa ukiwa na miaka 88.  Sijutii au kuogopa chochote, najiona nafanya haki tu.”
Mwanamke huyo aliyeonekana kuwa “mwenye furaha zaidi duniani” kwa mujibu wa marafiki zake alihamia Uingereza mwaka 2002 na akahitimu masomo kwenye chuo kikuu cha uhandisi cha Nottingham Trent nchini humo.
Mama yake anaishi Marekani na dada yake yuko Canada, ambapo kaka yake yuko Gillingham, Kent, Uingereza lakini kwa umbali wa kilomita 402 kutoka alipo.
 
Alipohitimu chuo kikuu Uingereza.
 
Picha nyingine enzi za uhai wake akiwa katika vazi murua.

No comments:

Post a Comment