flash3

Monday 7 January 2013

AVRIL KUTOKA KENYA AKANA KUTOKA NA DIAMOND


Msanii kutoka humu nchini alietoka na single yake "kitu kimoja" Avril,  amekua akitajwa kuwa na mahusiano na wanaume kadhaa tangu alipoingia katika game ya muziki.
 Miezi ya nyuma tetesi zilisema kuwa anatoka na co-host wa kiss 100 Jalang'o, kitu ambacho kilikuja kugundulika ni uongo

Ijumaa iliyopita kupitia mitandao ya jamii, story zilivuma kuwa Avril anatoka na Diamond na hasa ni baada ya kutokea kwa mara ya pili kwenye video za Diamond 
kesho na nataka kulewa.
Baada ya kumpata Avril juu ya tetesi hizi, kupitia mtandao wa kenyan-post.com, hiki ndicho alichokisema
"mimi na Diamond? hapana kabisa, sio chochote, ni marafiki tu.
Sikuwa msanii pekee alietokea katika video yake, alituomba tumpe sapoti katika video yake ya kesho na nataka kulewa ambazo zilitengenezwa na kurekodiwa na Ogopa Djs.
 Sijaenda Zanzibar na Diamond, nilikua peke yangu kwa wiki moja ya likizo, nashangaa nani ameanzisha hizi tetesi"

No comments:

Post a Comment