flash3

Wednesday 9 January 2013

KALI YA LEO: UHAMISHO WA VAN PERSIE KWENDA MAN U ULISABABISHA UGOMVI NA WATOTO WAKE

Mshambuliaji wa Manchester United amezungumza kwamba kuhamia United kulimletea mtafaruku baina yake na wanae wawili ambao ni washabiki wa kutupwa wa Arsenal. Katika mahojiano aliyoyafanya mwezi uliopita Persie anasema halikuwa jambo rahisi kwa wanae kukubaliana na ukweli kwamba anahama timu wanayopenda na kuhamia kwenye timu mahasimu, lakini kupata nafasi ya kucheza Man U ni nafasi adimu inayotokea mara moja kwenye maisha hivyo ilivyotokea nafasi ikabidi aitumie. Mke wa Van Persie pia anasema ilifikia kipindi mwanae aliwahi kumwambia anashindwa kumheshimu baba yake kwa kuhama Arsenal mara alipoona picha ya Van Persie na Sir Alex Ferguson. Kwa mengi zaidi angalia hiyo video hapo chini.      

No comments:

Post a Comment