flash3

Monday 28 January 2013

BREAKING NEWS:LULU KUACHIWA KWA DHAMANA

  Baada ya wanasheria wa msanii huyo ambao ni Peter kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe,  kutuma maombi ya dhamana ya kesi ya Lulu ili isomwe haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu mahabusu, sasa habari zilizotoka hivi punde kutoka mahakama kuu zinasema lulu ametakiwa kukamilisha masharti aliyopewa, ikiwa ni kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezi,  na wafadhili wawili kuweka bondi ya Shilingi mil 20 kila mmoja...masharti hayo yakikamilika leo hii ataachiwa huru kuwa uraiani.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.

No comments:

Post a Comment