flash3

Tuesday 24 April 2012

RAKIM ASEMA WASANII KAMA KANYE WEST WANAITAJIKA KATIKA MUZIKI WA HIP HOP.

 

 Akiwa katika game la Hip Hop kwa miaka 25

emcee Rakim, wasanii na mashabiki wamempa
 heshima kubwa emcee huyo kwa sanaa yake.
 Mwana Hip Hop amempa sifa nyingi Kanye West.
 Katika mahojiano na “The Atlantic”
The God emcee huyo amemsifu sana Kanye West
 kwa licha tu ya kuwa rapper pia ni memba wa jamii
ya hip hop, Alisema kama emcee na mtayarishaji wa
 mapigo ya muziki ameipeleka hip hop kwenye level
 nyngine, Ingawa bursts kutoka kwake inaonyesha
kwamba alivutiwa na notorious.

“ Nampenda Kanye West kwa hilo, kuwa producer,
kufanya zile beats kali na rapper anafanya hivyo
vyote ni mkali sana” alisema Ra. “ Nikiwa mahali
 alafu nikisikia ile ngoma yake ya “ Jesus walk” dah
 noma natulia nakuwa nataka mtu asinisumbue niisikilize
 ngoma hiyo ni kati ya ngoma zangu kali za
 Kanye West, haogopi kufanya ngoma ambazo
 zinavuka mipaka na kuongelea vitu ambavyo
 wasanii wengine wanaogopa kuimba” Alifunguka Rakim.
 Mwaka 2007 Rakim, Kanye West, Nas, KRS One
na Dj Premier walishirikiana kwenye bonge moja la
ngoma “Classic” katika kusherekea miaka 25 ya
 Nike Air force one sneaker.

No comments:

Post a Comment