flash3

Friday 27 April 2012

SUMA C AAHIDI KUTEKA CHATI ZA PWANI.............. 

Baada ya kuachilia Track yake mpya 'Thafash' sasa awaahidi mashabiki wake kuwa ameamua kuwapa vitu visafi, kwani hata kwa upande wa video ameamua kufanya na kampuni moja kubwa nairobi ambayo kwa sasa ameiweka kwa mabano.
Suma c ambaye ni kati ya wale wana muziki pwani ambao wamepata sifa baada ya kufanya Track kama Vile Bonge La Party na Wewe alizowashirikisha Escoba Babake na Lai Mtawalia  na kisha Ramadhan Ikipita......vibao vilivyo vuma sana, sasa adokeza kuwa hatarudi nyuma bali malengo yake ni kuvuka boda na kuhakikisha kuwa mziki wa Mombasa hauwi wa wakaazi wa Mombasa peke bali wa kote ulimwenguni.
akizungumza  katika Redio Pwani Fm Mombasa wakati alipokuwa na mahojiano na Dj Mafimbo mmiliki wa Mfb Ent, Suma amewaomba mashabiki kuukubali mziki wa pwani kwani ndio chanzo cha kuubeba na kuuza mbali.
wakati uo huo msanii huyo anayefanya kazi na Crack sound chini ya Producer Lai, aliwataja walanguzi wote wa fani hii ya muziki kuwa chuma chao kimotoni na anawaomba wadau kuingilia kati ili kunusuru fani pwani.

No comments:

Post a Comment