flash3

Friday 13 April 2012

RICK ROSS ASHINDWA KUTOKEA KWENYE SHOW BAADA YA MATATIZO YA KIAFYA.

Baada ya kukatisha show yake ya Houston na
Guyana, inasemekana ugonjwa uliokuwa ukimsumbua
 Rozay mwaka jana umerudi tena. Jumatatu gazeti la
Houston liliripoti kwamba Rick Ross ameshindwa
kutokea kwenye show iliyopangwa ifanyike April 7
Houston Bayou Music Centre. Mwandishi Marco Torres
wa gazeti hilo aliripoti Rozay hatofanya show
 kutokana na kuumwa ugonjwa wa seizure kwenye
 chumba cha hotel aliyofikia. HipHop-N-More, WENN.com
na vyanzo vingine vya habari vinaripoti kwamba Rozay
alishindwa pia kutokea kwenye "Easter Fest Rozay" show
 huko Guyana kutokana na uongozi wake kusema ilitokea
matibabu ya dharura ndo statement iliyotolewa kwa
Hits and Entertainment kampuni ya promosheni hapo
 Guyana ambao ndo waliandaa show hiyo.

Tukio kama hilo lilishatokea October 2011 wakati
 Rozay alipopatwa na ugonjwa huo akiwa kwenye
ndege akitokea Fort Lauderdale Florida, Rapper
huyo pia alishapata ugonjwa huo tena siku moja kabla
ya show ya Memphis Tennessee, Rick Ross amefuta
Tour zote za Ulaya na alikuwa aende Houston kabla
 ya matatizo hayo.
Uongozi wake umesema wako tayari kupanga siku
nyingine kwa ajili ya show hiyo
mara baada ya Rick Ross kuwa fresh.

No comments:

Post a Comment