flash3

Tuesday 17 July 2012

AFTER LONG WKND AT THE COAST OF KENYA WE R SORRY CHEGE APATA AJALI,afta show kibao nchini kenya


Msanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi kwa shughuli kadhaa za kimuziki.
katika umbea wetu na mashav kamera Chege amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana pikipiki katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata ajali hiyo , Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.…

Hivi ndivyo gari la Chege lilivyokuwa baada ya ajali
Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na pikipiki,Kupitia mahojiano hayo mafupi Chege amewatoa hofu mashabiki wake kuwa hali yake ni nzuri na yupo salama.
Staa wa bongo fleva Naseeb Abdul 'Diamond' amempa pole mwanamuziki mwenzie huyo wa Kigoma All Stars kwa kilichotokea na kuwataka wasanii wengine kumtia moyo Chege
"Nampa pole mwanangu Chege Chigunda kwa ajali mbaya ya gari aliyopata ,Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote yaliyotokea" alisema Diamond
.

No comments:

Post a Comment