flash3

Tuesday 31 July 2012

AUNTY EZEKIEL KUFUNGA NDOA MWEZI OCTOBER

ILE kasumba kwamba hakuna msanii wa bongo muvi anayeweza kuolewa na kudumu ndani ya ndoa, inatarajia kufutwa na msanii Aunty Ezekiel, ambaye anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi wake anayeishi Dubai ambako ndiko atakoenda kuishi baada ya kufunga ndoa.

Aunt Ezekiel anaelezea kuwa ni jambo la busara
juu ya maisha yake na filamu kwa ujumla ambapo. Huku akisisitiza kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo  kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye maisha.
“Nilikuwa kimya juu ya ishu hii lakini ninachotaka kusema ni kwamba mambo yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu nawahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua.

mrembo Huyu  asema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa, kwani ni jumapili iliyopita vikao vilianza kushughulika.

Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

No comments:

Post a Comment