flash3

Friday 27 July 2012

AY NA JASON DERULO KWENYE SAKAFU MOJA THIS SATURDAY.


Ay.
Kwa mara nyingine tena jumamosi ya July 28 2012 Ay kutoka Tanzania anashare stage moja na International Super Star Jason Derulo kwenye ardhi ya Paul Kagame.
Hii ni mara ya kwanza Ay kuperfom kwenye show na Jason Derulo lakini mpaka sasa tayari amepiga show moja na mastaa wengine kama Sean Kingston, Miss Eliot, Akon, Wyclef, Shaggy na wengine kwenye nchi tofauti tofauti.
Ay amethibitisha kupitia millardayo.com kwamba kwa sasa malipo yake ni dola elfu kumi za Kimarekani zaidi ya milioni 15 za kibongo kwa show zake za nje ya Tanzania, mpaka sasa akiwa ameshapiga showz zaidi ya kumi nje ya nchi kwa mwaka huu pekee.
Show zake nyingine za nje zijazo ambazo zipo kwenye list ya mwaka huu ni pamoja na Zimbabwe, Kenya na Sudan.

.
Jason Derulo anakua msanii mwingine staa kutoka Marekani kufika Rwanda ikiwa ni miezi michache tu toka nchi hiyo itembelewe na Trey Songs ambae alikwenda kuperform kwenye private party ya birthday ya mtoto wa Rais Paul Kagame.

No comments:

Post a Comment