flash3

Tuesday 4 September 2012

KUHUSU DROGBA KWENDA LIVERPOOL.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers kuna uwezekano akamsajili mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ambae stori zimemuhusisha kukaribia kuiacha club yake mpya ya Shanghai aliyojiunga nayo miezi miwili na nusu iliyopita.
Rodgers amekaririwa akisema yuko tayari kuangalia namna ya kujipanga kulishusha hili jembe Anfield au Michael Owen ambae hana timu kwa sasa.
Liverpool walipoteza game dhidi ya Arsenal home kwao kwa kuchapwa 2-0 na wamejikuta kwenye mwanzo mbaya kwenye historia ya ligi kuu England kwa zaidi ya miaka 50, hawajawahi kuwa na mwanzo kama huo.
Hata hivyo Kampuni inayomsimamia Didier Drogba imekanusha taarifa za kukatishwa kwa mkataba wake na club ya shanghai shenhua lakini bado haijulikani itakuaje baada ya viongozi wa club ya shenhua kuwa na mgogoro hali ambayo inaweza kuilazimu club kukatisha mkataba wake.

No comments:

Post a Comment