flash3

Saturday 15 September 2012

MUONEKANO MPYA WA SERENGETI FIESTA JINSI ULIVYOTIKISA UWANJA WA JAMHURI MKOANI DODOMA BHASSSSSSS ........

 Ni moja kati ya wasanii wanaoimba miondoko ya RNB huko Tanzania na pia mashabiki wa muziki wa bongo fleva wanamkubali sana pale anapoonyesha hisia zake wakati anapoimba huyu si mwingine anafahamika kwa jina la Ben pol.
Msanii huyu naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wametikisha lile jukwaa la serengeti fiesta mkoani dodoma usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya jamhuri.

                                                                           Ben pol
 Wakazi wa mkoa wa Dodoma walikusanyika kwa pamoja katika kiwanja cha jamhuri usiku wa kumkia leo  kushuhudia jinsi muonekano mpya na burundani ile ile ya serengeti fiesta jinsi inavyotoa burundan ya uhakika kabisa kutoka kwa wasanii mbalimbali.
   Rich Mavoco naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wametikisa vibaya  lile jukwaa la serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri usiku wa kuamkia leo.
                                                          Rich Mavoko.....
      Supa nyota anayefahamika kwa jina la Young killer akionyesha vitu vyake katika jukwaa la serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri usiku wa kuamkia leo.
 Ni moja kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika muziki wa bongo fleva  anafahamika kwa jina la Dyna.
Msanii huyu naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao walitoa burudani ya kutosha katika serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri usku wa kuamkia leo.

Ni moja kati ya wasanii wanaotokea katika jumba la vipaji hapa Tanzania THT huyu si mwingine anajulikana kwa jina la Linah naye alikuwa katika tamasha hilo akionyesha vitu vyake katika jukwaa la serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri.
  Shetta akionyesha juhudi zake katika jukwaa la serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri usiku wa kuamkia leo.
 Ni moja kati ya wasanii ambao wamepiga show zaidi ya sita za fiesta serengeti  mwaka huu.Huyu si mwingine namzungumzia Recho naye alikuwa ni mmojawapo wa kuonyesha muonekano mpya katika jukwaa la serengeti fiesta mkoani Dodoma katika viwanja vya jamhuri usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment