flash3

Saturday 10 November 2012

BEN POL AWATEMA OGOPA VIDEO KATIKA KUFANYA VIDEO YAKE MPYA"PETE"

Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama Ben Pol anatamba na ngoma kadhaa kali za RNB kama Nikikupata,Samboira,Pete, na ngoma zingine kali alizopewa collabo hapa Bongo sasa.
Latest info kutoka kwa Ben pol  kama unakumbuka kipindi cha nyuma alishawahi kuzungumza kwamba video yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la Pete alikuwa anatarajia kwenda nchini Kenya kuifanya shooting  na Production ya Ogopa
Sasa leo baada ya kupiga naye Story za hapa na pale ameamua kutiririka na kuweka wazi baada ya kumuliza vipi kuhusiana na video hiyo alisema kwamba ameamua kufanya na Adamu Juma kwani Director huyu ametokea kumkubali baada kufanya powa video yake inayofahamika kwa jina la Nikikupata.Baada ya kumaliza kusema hivyo pia aliamua kusema kwamba Jumapili inayokuja ndiyo anatarajia kuanza shooting na Director Adamu Juma kutoka Next Level.@Info kamili by Ben pol Artist.

No comments:

Post a Comment