flash3

Tuesday 13 November 2012

R.I.P MARIAM KHAMIS

 Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam Khamis almaarufu kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kujifungua .

Mariam Khamis umauti umemkumba akiwa anaimba kundi la TOT plus lakini enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab likiwemo East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.

Khamis Muhidini Shomary baba wa marehemu amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa hapo kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.info kamili baba mzazi wa Mariam Khamis.

No comments:

Post a Comment