flash3

Tuesday 21 August 2012

BRAND NEW TRACK KUTOKA KWA PROFESSOR J NA DULLY SYKES "HELLOW" UTAKUWA UNAPATA KUISKIA NDANI TAFRIJA REMIX....


Kama nilivyoahidi kupitia post hii hapa, Professor Jay(The Heavy Weight MC) ameamua kuingiza mtaani(kupitia kila aina ya media inayoweza kuwafikia wananchi na mashabiki wa muziki) single inayokwenda kwa jina Hellow. Hii inakuwa single ya tatu kutoka katika album ya JaySco Dagama ambayo ingawa bado hajaamua kuitoa rasmi,ni wazi kabisa kwamba pengine itakuwa album bora kabisa kuwahi kutolewa nchini Tanzania na msanii kutoka kizazi kinachoitwa “Kizazi Kipya” au New Generation.
Hellow unatoka katika kipindi muafaka.Kama unafuatilia sindimba za starehe nchini Tanzania,kilichopo kwenye kona ni msimu mnene wa Fiesta.Hellow,bila shaka,inalenga katika kuhakikisha kwamba,mtaani kila mtu anamwambia mwenzake Hellow.
Hii ni production kutoka kwa Dully Sykes ambaye bila shaka utakubaliana nami kwamba ameitendea haki vilivyo chorus ya wimbo huu.Usikilize Hellow

No comments:

Post a Comment