flash3

Wednesday 15 August 2012

MSHINDI WA TUSKER 2012 NA KAULI YA KWANZA KWENYE AMPLIFAYA, ATAJA JINSI PESA ZILIVYOMBADILISHA!

 
Ruth Matete na Jaji Ian
Mshindi wa Tusker Project Fame 2012 Mkenya Ruth Matete kwa mara ya kwanza ameongea kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutaja mabadiliko yaliyotokea kwenye maisha yake kutokana na milioni 5 za kenya alizokabidhiwa kama sehemu ya zawadi.
Ruth amesema kwanza sasa hivi hapandi daladala maarufu kama matatu, pia anatembea na mlinzi kila mahali atakapokwenda.. anafanya kama wanavyofanya mastaa wengine wakubwa wa dunia, hiyo ni kutokana na ulinzi wake binafsi baada ya kupata huo umaarufu kupitia Tusker Project fame.

Matatu ambazo zamani Ruth alikua amezoea kuzipanda sana lakini toka ameshinda TPF imebidi aache kutokana na ustaa.
Amesema sasa hivi hawezi kununua vifaa vya muziki kutokana na hizo pesa kwa sababu hajui kupiga chombo chochote cha muziki lakini anaweza kuziwekeza kwenye sehemu nyingine japo hajajua ni nini atakachofanya.

No comments:

Post a Comment