flash3

Tuesday 28 August 2012

Vurugu zaingia siku ya Pili Hapa Jijini..........

Rais Mwai Kibaki anatarajiwa kufika mjini Mombasa Alhamisi kufungua rasmi maonyesho ya kilimo ya Mombasa, wakati ambapo mji huu unashuhudia vurugu zinazosababishwa na vijana wanaopinga kuuawa kwa mhubiri wa dini ya kiislamu Aboud Rogo Mohammed.
Mapema Leo, ghasia zimezuka upya katika mitaa ya Majengo, Saba Saba na Makupa ambapo watu watatu wamejeruhiwa vibaya.
Mkuu wa polisi mkoani Pwani Aggrey Adoli amekanusha vikali madai kuwa mke wa mhubiri huyo ameaga dunia akisema amelazwa.
Haniya Saaid Sagaar anauguza jeraha la risasi kwenye mguu wake. Aidha, Adoli amewakosoa wafwasi wa muhubiri huyo kwa kuwanyang'anya maafisa wa polisi mwili wa marehemu na hivyo kuhujumu uchungunzi wa kifo hicho.
Polisi wamekuwa wakikabiliana na vijana wanaozua vurugu katika barabara za Nkrumah, Nyerere, Digo, Posta na Moi jijini humu. Hali hiyo imesababisha maduka kadhaa kufungwa baada ya wamiliki kuhofia usalama wao huku wengine wakiwa wameporwa pesa na mali nyinginezo. `

No comments:

Post a Comment